Kwanza kabisa jaribu kuebuka kubananisha vitu wakati unaweza ukatumia sehemu kama Ukuta wako kwa kuutenezea shelves nzuri ambazo zitabeba vitu kama vitabu,flower vases,frame za picha n.k basi ni vyema kutafuta designer mzuri ili aweze kuifanya hiyo kazi kwani itakupunguzia wingi wa vitu visivyokuwa na mpangilio mzuri..!
Pia mfano mwingine mkubwa ambao watu wengi huanza nao ili kuifanya nyumba au chumba chako kionekane kikubwa kwa namna moja au nyingine...hii njia ya kuchagua rangi ya kupaka ukutani...na pia jinsi yakumatch hiyo rangi na rangi za furniture zako.
Pili jifunze kupanga vyombo vya ndani mfano kwenye sebule Kochi,viti na meza vizuri kulingana na design ya sebule yako, ambapo decoration yako ita-matter sana hapo consider vitu kama color, accessories na vitu vingine vidogodogo.
Njia nyingine jaribu kununua furniture ambazo zinaifadhi vitu zaidi ya kimoja..mfano kama ni meza iwe na drawers hivi au kama kitanda kiwe na drawers kwa chini ili uwe na uwezo wakuweka vitu vyako kama Nguo n.k.
Nahivyo basi tumia mbinu hizi chache kwa vyumba vyako ikiwemo chumbani,study room,jikoni hata chooni.
Post a Comment