Pia kwenye Dressing Table ni vyema kudesign kulingana na matumizi yako..weka kioo kikubwa chakutosha kujitazama na pia dressing table yako iwe na drawer za kutosha uhifadhi vipodozi kuzingatia pia aina ya vipodozi/ cosmetics unazotumia hii ni kutokana huwezi kuweka kila kitu juu ya dressing table yako..weka pia accessories zako mfano..pete, ear-rings au bangili zako kwenye pochi maalumu kisha hifadhi kwenye droo! hii husaidia zisiharibike kwa urahisi au kuibiwa kama itatokea, pia hifadhi vifaa vya kutengeneza nywele kwenye drawers mfano machanuo na vibanio!
Kila mwanamke hupenda nyumba ipendeze basi zingatia pia ku-decorate Dressing Table yako kwa kuweka hata chupa ya ua zuri juu yake..frame ya picha au other accessories..!
Post a Comment