0
Tukiendelea na mada ya jinsi ya kupamba kuta za room yako leo tuangalie kwa wale wenye nyumba zenye corridor au hallway huwa wanapamba kwa kutumia nini ..kwa nyumba nyingi tumeona sehemu kubwa ya kuupendezesha ukuta ni pamoja na kutumia frames za picha ambapo hapa frames zake zinatakiwa kuwa kubwa ikiwa utakuwa na eneo kubwa la ukuta...vile vile ni vyema kujua  na kuzingatia ukubwa wa corridor yako kwani kuna corridor pana na zile nyembamba.

Vile vile kuna upambaji wa kuta za hallway kwa kutumia kioo kama pambo,au taa maalumu zijulikanazo kama lamp shade za ukutani ili kuongeza rangi yenye kuvutia wakati wa usiku.

Hivyo ni uchaguzi mzuri kujua nini kunafaa kuupendezesha ukuta wa nyumba yako kwa kutumia mifano hiyo michache! Na kama unaushauri,maoni na hitaji lolote kutoka kwetu kupitia mada zetu please usisite kuwasilana nasi kwa kuniandikia.

Email~whitewings.homedecors@gmail.com








Post a Comment

 
Top